Dhifa
KES 383
Availability: In stock
Quick overview
Dhifa ni diwani ya mashairi yenye sauti kali na inayoacha mwangwi mkuu kwenye sikio la msomaji...
Dhifa ni diwani ya mashairi yenye sauti kali na inayoacha mwangwi mkuu kwenye sikio la msomaji. Ni diwani inayofichua uchafu na taksiri zilizojaa katika maisha ya watawala na viongozi ambao wametiwa shemere na ulafi kwenye dhifa ya kuyamega mataifa yao kwa uroho huku raia wakiendelea kuteseka, na hata kuhongera ulaji huo. Ni sauti ya tashtiti inayozipekecha hisia za ndani za msomaji.
Sauti inayomchochea kuitazama jamii yake na kuyatazama maisha yake kwa jicho la ndani. Hii ni diwani inayotumia ucheshi, sauti na tashtiti kuuwasilisha ujumbe kwa raia wa nchi zetu katika
enzi hii ya utandawazi.