Kaza Macho
Availability: In stock
Quick overview
Kaza Macho ni mkusanyiko wa mashairi yanayoonyesha upeo wa juu...
Kaza Macho ni mkusanyiko wa mashairi yanayoonyesha upeo wa juu wa kipawa cha utunzi alichonacho mtunzi wa mashairi yaliyomo. Mashairi hayo yametumia lugha ya kitamathali itakayomwachia msomaji taathira ya kudumu kwa namna yanavyozigusa hisia mbalimbali za msomaji.
Mashairi yanayopatikana katika diwani hii yanaangazia mawanda yote ya maisha ya watu kwa jumla, hasa katika bara la Afrika, yakipiga darubini ndoto na matamanio yao, kadhia za maisha yao kijamii, kisiasa, kiuchumi na kihistoria. Maisha yenyewe hayakosi migogoro, na watu wakiwa katika mapambano ili kujikwamua kutokana na hali anuwai zinazotishia kuhujumu uhuru, amani na maendeleo yao.
Hii ni kazi ambayo hataiweka chini yeyote aanzapo kuisoma hadi atakapolisoma shairi la mwisho.