Mwenge wa Uandishi
Availability: In stock
Quick overview
A must have companion for composition writing...
Provides good tips for creative writing and functional. Rich in examples, systematic and exemplary ordered.
Mwenge wa Uandishi: Mbinu za Insha na Utunzi ni kitabu kinachoelezea na kufafanua aina tofauti na sifa za insha kama: insha ya maelezo, insha ya mazungumzo, insha ya mawazo, insha ya mdokezo na insha ya methali kwa kina ambacho hakipatikani katika vitabu vingi vya aina hii. Isitoshe, mifano ya kuafiki na ya kutosha imetolewa.
Kwa mara ya kwanza katika uandishi wa insha ya Kiswahili, suala la aya linachunguzwa kwa kina kikubwa. Aya ni kipengele muhimu na cha kimsingi katika muundo wa maandishi. Je, aya huanza vipi? Aya hujengwa na nini? Msomaji hujuaje kuwa anatoka aya moja hadi nyingine? Maswali haya na mengine yamejibiwa katika kitabu hiki chenye undani wa kupigiwa mfano. Aidha kitabu hiki kimeshughulikia aina zote za maandishi yanayoweza kupatikana.