Sumu ya Bafe
KES 321
Availability: In stock
Quick overview
A play on the deception of political leaders in a postcolonial setting...
Sumu ya Bafe ni tamthiliya inayotumia sitiari nzito kuichunguza historia ya mahusiano baina ya viongozi na watawaliwa katika jamii inayopigwa na wimbi la siasa ya ulimwengu wa leo.
Ni tamthiliya inayobainisha unafiki, ubarakala na ubinafsi wa tabaka tawala kwa kuonyesha jinsi linavyoweza ‘kuiteka nyara’ lugha na kuubatilisha ukweli dhahiri kwa manufaa ya kundi dogo.
Hata hivyo, katika fondogoo iliyopo katika jamii, bado kuna matumaini. Hii ni tamthiliya iliyojaa ucheshi na tashtiti inayokereketa.