Kamusi ya Semi
Availability: In stock
Quick overview
Kamusi ya Semi: Maana na Matumizi ni kanzi iliyosheheni semi nyingi...
Kamusi ya Semi: Maana na Matumizi ni kanzi iliyosheheni semi nyingi kutoka maeneo tofauti tofauti ya Afrika Mashariki na Kati kunakozungumzwa Kiswahili. Kanzi hii aidha imejumuisha semi mpya ambazo zimeibuka kutokana na ukuaji na kuimarika kwa lugha ya Kiswahili. Kamusi hii itawanufaisha wapenzi wa lugha ya Kiswahili na kuwa mwenza muhimu kwa walimu na wanafunzi wa lugha ya Kiswahili popote walipo.
Sifa zinazobainisha kamusi hii ni:
• Idadi kubwa ya semi ya zaidi ya 4900,
• Visawe zaidi ya 700,
• Maana na mifano safi ya matumizi ya semi mbalimbali.
• Ulinganishi wa semi zilizo na maana moja.
Kamusi hii itakuwa nyenzo muhimu na msingi wa kuujenga umilisi wako wa lugha ya Kiswahili.