Mvuvi Maskini na Waziri na Hadithi Nyingine ni kitabu ambacho kina visa vinne vya kuchangamsha na vilivyosimuliwa kwa ustadi mkubwa. Kwanza kuna tajiri aliyetaka kuchorwa na mchoraji. Je, matokeo yake yalikuwa nini? Je, unajua maana ya kukiona cha mtema kuni? Soma kisa cha ‘Mkata Kuni’ ujue maana yake. Kisa cha tatu kinamhusu waziri aliyekuwa na tamaa na mvuvi. Je, ni nini kilichompata? Kisa cha mwisho, ‘Punda Wawili’ ni kisa kilichojaa mafunzo kemkem.