Books Search

Nagona

KES 377

Availability: In stock

Quick overview

Nagona ni riwaya inayothibitisha upevu wa falsafa ya Kezilahabi kuhusu dhana ya maisha...

COM_VIRTUEMART_CART_QUANTITY_ME:

Nagona ni riwaya inayothibitisha upevu wa falsafa ya Kezilahabi kuhusu dhana ya maisha. Katika riwaya hii, maisha yanasawiriwa katika mtazamo wa dhihaka na kejeli. Ndiyo maana mwandishi anatega kitendawili kwamba waliobahatika kuishi, “…walikufa katika vurumai.

Walikufa wakicheka hali wameshikilia mbavu zao kwa vichomi. Baadhi walikanyagwa kanyagwa, wakafa wakicheka. Wengine… walitumbukia katika kisima cha ndoto zao wakafa kwa wingi wa ndoto walizokunywa….”

Hakika kitabu hiki kinaweza kutazamwa kama ‘pacha wa riwaya ya Mzingile kutokana na kushabihiana kwa dhamira zake zinazochambua suala gumu la kifalsafa lihusulo maana ya maisha. Hii ni riwaya itakayopendwa na wanafasihi wapevu, mashuleni, vyuoni na kadhalika.

Contact us

  • icon
    Address : Vision Plaza 3rd Floor, Mombasa road, Nairobi-Kenya.
  • icon
    Telephone : +254 20 2619565
    Mobile : +254 720 059511