Books Search

Mtambo wa mauti

KES 383

Availability: In stock

Quick overview

Anaitwa Mona Lisa. Msichana mwenye sura ya malaika...

COM_VIRTUEMART_CART_QUANTITY_ME:

Anaitwa Mona Lisa. Msichana mwenye sura ya malaika na umbo la malkia. Mona Lisa anafanikiwa kuutikisa ujabali wa Joram Kiango hata anajikuta akiamua kustarehe naye. Lakini pale anapokurupuka usiku wa manane na kumkuta Mona Lisa akiwa maiti, tundu la risasi likivuja damu kifuani mwake, ndipo Joram Kiango anapojikuta katikati ya mkasa mzito, wa kutisha, ambao hajapata kukutana nao maishani.

Mkasa ambao vitisho nyake vinaongezeka kila dakika hasa pale Mona Lisa aliyekufa jana anapotokea leo, tena katika kila maficho ya Joram Kiango. Na kila anapotokea, maisha ya
watu wengi, wenye hatia na wasio na hatia, yanaendelea kuteketea.

Je, Mona Lisa ni binadamu wa kweli, jini au malaika? Ni miongoni mwa maswali ambayo msomaji atajiuliza anaposoma hadithi hii ya kusisimua, hadithi ambayo utakapoanza kuisoma, hutataka kuiacha kamwe hadi tamati.

Contact us

  • icon
    Address : Vision Plaza 3rd Floor, Mombasa road, Nairobi-Kenya.
  • icon
    Telephone : +254 20 2619565
    Mobile : +254 720 059511